Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 109

Al-An'aam 6:109

الأنعام

وَأَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ لَئِن جَآءَتْهُمْ ءَايَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا ٱلْـَٔايَـٰتُ عِندَ ٱللَّهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَآ إِذَا جَآءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vyao vikali zaidi, kuwa ikiwajia Ishara, bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Ishara hizo ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na ni nini kitawajulisha kuwa zikija, hawataamini?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara wataiamini. Sema: Ishara ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa zitapo kuja hawato amini. [109]

[109] Na washirikina waliapa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwajia Ishara ya kuiona katika Ishara walizo zitaka, basi yakini hiyo itakuwa ni sababu ya kuamini kwao. Sema ewe Nabii: Ishara hizi ziko kwa Mwenyezi Mungu. Yeye peke yake ndiye Mwenye madaraka juu yake hizo ishara. Mimi sina uweza wa hayo. Nyinyi Waumini, hamjui ninayo yajua Mimi. Hata zikiwajia Ishara hizi hawataamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waliapa washirikina hawa viapo vya mkazo, «Lau Atatujia Muhammad kwa alama yenye miujiza, tutayaamini yale aliyoyaleta.» Sema, ewe Mtume, «Kuja kwa miujiza yenye kushinda kunatokana na Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Yeye Ndiye Mwenye uwezo wa kuileta Akitaka.» Na nilipi liwajulishalo nyinyi, enyi Waumini: huenda miujiza hii ikija hawataiamini hawa washirikina?».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net