Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 107

Al-An'aam 6:107

الأنعام

وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشْرَكُوا۟ ۗ وَمَا جَعَلْنَـٰكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ

Maana

Na lau Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelimshirikisha. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao. [107]

[107] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka wamuabudu Yeye peke yake angeli walazimisha kwa nguvu na kwa uweza wake. Lakini Yeye amewaachilia watumie khiari yao. Na Sisi hatukukufanya wewe kuwa ni muangalizi wao, ukiwahisabia vitendo vyao. Wala wewe hukulazimishwa kuwa usimamie kuwapangia na kuwatengenezea mambo yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Allah Mtukufu angalitaka wasishirikishe hawa washirikina hawangalishirikisha, lakini Yeye, Aliyetukuka, ni Mjuzi wa yatakayokuwa ya ubaya wa uchaguzi wao na kufuata kwao matamanio yaliyopotoka. Na hatukukufanya wewe ni mchunguzi wa kuwatunzia matendo yao wala hukuwa ni msimamizi wao wa kuwapangia maslahi yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net