Al-An'aam 6:106
الأنعامٱتَّبِعْ مَآ أُوحِىَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ ٱلْمُشْرِكِينَ
Fuata yale yaliyofunuliwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Na jitenge na washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Fuata uliyo funuliwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hapana mungu ila Yeye. Na jitenge na washirikina. [106]
[106] Ewe Nabii! Fuata wahyi ulio kujia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye kumiliki na kuendesha mambo yako. Hakika Yeye peke yake ndiye Mungu anaye stahiki kut'iiwa na kunyenyekewa. Basi shikamana na ut'iifu wake, wala usibali inadi za washirikina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Fuata, ewe Mtume, wahyi tuliokuteremshia, wenye maamrisho na makatazo ambayo, kubwa lake ni kumpwekesha Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, na kuita watu huko. Na usijali ushindani wa washirikina na madai yao ya urongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net