Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 105

Al-An'aam 6:105

الأنعام

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَـٰتِ وَلِيَقُولُوا۟ دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُۥ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Maana

Na namna hivyo tunazileta Aya mbalimbali, na wao wakwambie: 'Umesoma.' Na ili tuyabainishie watu wanaojua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanao jua. [105]

[105] Na mfano wa uchambuzi kama huu wa pekee katika kueleza dalili za maumbile, ndivyo tunavyo eleza Ishara zetu katika Qur'ani kwa njia namna kwa namna na kwa mbali mbali, ili kusimamisha hoja za kuwashinda hao wapingao. Kwa hivyo wao hawapati ila kuzua uwongo, wakakutuhumu kuwa haya umejifunza kwa watu, wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nasi tunabainisha haya uliyo teremshiwa, nayo ni Haki isiyo athirika na kipendacho moyo, kwa ajili ya watu ambao wanayo ielewa Haki na wanainyenyekea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tulivyowafafanulia washirikina, katika hii Qur’ani, hoja zilizo wazi juu ya jambo la kumpwekesha Allah Mtukufu, utume na marejeo ya Kiyama, tunawafafanulia hoja katika kila wasichokijua. Na hapo wanasema urongo, «Umejifunza kutoka kwa watu wa Kitabu!» Na ili tufafanue haki, kwa kuzileta aya, kwa watu wanaoijua na kuikubali na kuifuata, nao ni waliomuamini Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kile alichoteremshiwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net