Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 104

Al-An'aam 6:104

الأنعام

قَدْ جَآءَكُم بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَنْ عَمِىَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ

Maana

Hakika zimekwishawajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, mwenye kuona, basi ni kwa faida yake mwenyewe. Na mwenye kupofuka, basi ni hasara yake. Wala mimi si mtunzaji wenu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu. [104]

[104] Ewe Nabii! Waambie watu: Zimekwisha kujieni kutoka kwa Muumba wenu na Mwenye kumiliki mambo yenu yote, hoja na maelezo wazi katika hii Qur'ani. Hizo zinakuangazieni Njia ya Haki. Basi mwenye kunafiika kwazo, manufaa ni yake mwenyewe. Na mwenye kujitenga nazo, basi amejidhuru mwenyewe! Wala mimi si mlinzi wenu, bali mimi ni Mjumbe ninakufikishieni niliyo tumwa kwenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mmejiwa na hoja zilizo wazi kutoka kwa Mola wenu, mnaonea nazo uongofu na upotevu, miongoni mwa zile zilizokusanywa na Qur’ani na akaja nazo Mtume, rehema na amani zimshukiye. Basi mwenye kufunukiwa na hoja hizi na akayaamini yale yanayoelekezwa nazo, faida yake itamfikia mwenyewe. Na yule ambaye hakuuona uongofu baada ya hoja kumfunukia, basi amejikosea mwenyewe. Na mimi si mtunzi wa kudhibiti matendo yenu. Mimi ni mfikishaji tu. Na Allah Mtukufu Anamuongoza Anayemtaka na Anampoteza Anayemtaka kulingana na ujuzi Wake na hekima Yake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net