Al-An'aam 6:103
الأنعاملَّا تُدْرِكُهُ ٱلْأَبْصَـٰرُ وَهُوَ يُدْرِكُ ٱلْأَبْصَـٰرَ ۖ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلْخَبِيرُ
Macho hayawezi kumzunguka, naye anayazunguka macho. Naye ni Mjua siri, Mwenye habari zote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari. [103]
[103] Macho hayamuoni dhati yake, na Yeye anajua undani wa macho na vyenginevyo. Naye ni Mjuzi hakimpotei kitu, ni Mwenye khabari za kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Macho hayamuoni Allah Mtukufu ulimwenguni. Ama kwenye nyumba ya Akhera, Waumini watamuona Mola wao bila kumuenea. Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, anayafikia macho na kuyazunguka, na kuyajua vile yalivyo. Na Yeye ni Al-Laṭîf (Mpole) kwa mawalii Wake, Anayejua mambo yote hata yenye upeo wa udogo, Al-Khabîr (Mtambuzi) Anayejua mambo ya ndani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net