Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 102

Al-An'aam 6:102

الأنعام

ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَـٰلِقُ كُلِّ شَىْءٍ فَٱعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ وَكِيلٌ

Maana

Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi, hakuna mungu isipokuwa Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu. [102]

[102] Huyo aliye sifika kwa sifa za ukamilifu ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye, Muumba wa kila kitu vilivyo kuweko, na vitavyo kuwa. Basi ni Yeye tu Mwenye kustahiki kuabudiwa. Basi muabuduni Yeye, na Yeye peke yake ndiye Mwenye kutawala kila kitu na kila jambo. Marejeo yote ni kwake tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huyo, enyi washirikina, Ndiye Mola wenu, Aliyeshinda na kutukuka; hapana Mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye; Mwenye kuumba kila kitu. Basi mfuateni na mumnyenyekee kwa kumtii na kumuabudu. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mtegemewa na ni Mtunzi, Anayaendesha mambo ya viumbe vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net