Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 101

Al-An'aam 6:101

الأنعام

بَدِيعُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُۥ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُۥ صَـٰحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَىْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Yeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke? Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu. [101]

[101] Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi bila ya kuwa na kiigizo kilicho tangulia, vipi awe na mwana, kama wanavyo dai hawa, na hali Yeye hana mke, naye ndiye aliye umba vitu vyote? Miongoni mwa vitu hivyo ni hao wanao wafanya washirika wake. Naye ni Mjuzi wa kila kitu, na anawahisabia wasemayo na watendayo, na ni Mwenye kuwalipa kwa kauli yao na vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Aliyezipatisha mbingu na ardhi na vilivyomo humo, kwa namna isiyokuwa na mfano uliotangulia. Vipi Awe na mtoto, na hakuwa na mke? Ametukuka Allah Mtukufu kutukuka kukubwa na yale wanayoyasema washirikina, Na Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu kutokana na hali ya kutokuwako na hakuna chochote chenye kufichika Kwake katika mambo ya viumbe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net