Al-An'aam 6:100
الأنعاموَجَعَلُوا۟ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا۟ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَـٰتٍۭ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ
Lakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu zaidi ya hayo wanayomuelezea kwayo!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali Yeye ndiye aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo mbandikiza nayo!. [100]
[100] Juu ya dalili hizi makafiri wamewafanya Malaika na mashetani ni washirika wa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye aliye waumba hao. Haiwafalii kujua hayo wakamuabudu asiye kuwa Yeye, naye ndiye aliye waumba Malaika na mashetani. Haitakikani wawaabudu hao nao wameumbwa kama wao!! Na hawa makafiri wakambunia Mwenyezi Mungu wana. Wakristo wakadai kuwa Masihi ni mwana wa Mungu, na baadhi ya washirikina wa Kiarabu wakadai kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Na huo ni ujinga, kutokuwa na ilimu! Mwenyezi Mungu Mtukufu ameepukana na hayo wanayo muambatisha naye Subhana!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa washirikina wamefanya majini ni washirika wa Allah Mtukufu katika ibada, kwa kuitakidi kwao kuwa wao wanaleta manufaa au madhara, na hali Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Amewaumba wao na wanavyoviabudu kutoka kwenye ‘adam (hali ya kutokuwako). Basi ni Yeye Aliyepwekeka kwa kuumba, Peke Yake, na inapasa Apwekeke kwa kuabudiwa Peke Yake, Asiye na mshirika. Na kwa kweli, hawa washirikina walisema urongo kumzulia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, walipomnasibishia Yeye watoto wa kiume na wa kike, kwa kutojua kwao sifa Zake za ukamilifu zinazompasa. Ametakasika na kuwa juu ya yale ambayo walimnasibisha nayo washirikina, ya urongo na uzushi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net