Al-Mujaadila 58:9
المجادلةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا تَنَـٰجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَـٰجَوْا۟ بِٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَمَعْصِيَتِ ٱلرَّسُولِ وَتَنَـٰجَوْا۟ بِٱلْبِرِّ وَٱلتَّقْوَىٰ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِىٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Enyi mlioamini! Mnaponong'ona, msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezeni kwa kutenda mema na kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mnapo nong'ona msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezane kwa kutenda mema na kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote. [9]
[9] Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Mnapo sema siri, basi msiwe mkisema siri katika mambo ya madhambi, na kufanya uadui, na kwenda kinyume na Mtume. Semeni siri katika mambo ya kheri, na kuepukana na madhambi. Na mwogopeni Mwenyezi Mungu ambaye kwake Yeye tu, si kwengineko, ndio mtakusanywa baada ya kufufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini (Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo)! Mnapozungumza baina yenu kwa siri, msizungumze maneno ya dhambi au yenye uadui kwa wengine msiokuwa nyinyi au yanayoenda kinyume na amri ya Mtume. Na zungumzeni yale yenye kheri, utiifu na wema, na muogopeni Allah Mtukufu kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, Kwani Kwake Yeye Peke Yake ndipo mtakaporudi na matendo yenu yote na maneno yenu Aliyowadhibitia, na Atawalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net