Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 8

Al-Mujaadila 58:8

المجادلة

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نُهُوا۟ عَنِ ٱلنَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا۟ عَنْهُ وَيَتَنَـٰجَوْنَ بِٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَمَعْصِيَتِ ٱلرَّسُولِ وَإِذَا جَآءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ ٱللَّهُ وَيَقُولُونَ فِىٓ أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا ٱللَّهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Kwani huwaoni wale waliokatazwa kunong'onezana, kisha wakayarudia yale yale waliyokatazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: 'Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani huwaoni wale walio katazwa kunong'onezana kisha wakayarudia yale yale waliyo katazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyo kuamkia Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo? Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje! [8]

[8] Ewe Mtume! Huwaoni hao walio katazwa kufanya njama za siri wao kwa wao kwa mambo ya kutia shaka katika nyoyo za Waumini, kisha wakayarejea yale yale waliyo katazwa? Na wanafanya njama kwa madhambi wanayo yatenda, na uadui wanao uazimia, na uasi dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wanapo kuja kwako wanakuamkia kwa kauli ya kupotoa, sivyo anavyo kuamkia Mwenyezi Mungu. Na wao husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tunayo yasema ikiwa huyu ni Mtume kweli? Inawatosha hao Jahannamu. Wataingia humo waungue kwa moto wake. Na marejeo maovu yalioje marejeo yao. Ilikuwako sulhu baina ya Waislamu na Mayahudi katika mji wa Madina. Na ikawa akipita mtu katika Waislamu kwao Mayahudi hunong'ona wao kwa wao ili adhani yule Muislamu kuwa wao wanapanga njama za kutaka kumuuwa, au lolote la kumdhuru apate kugeuza njia asiwapitie tena. Mtume s.a.w. akawakataza hayo, lakini hawakuacha mtindo wao, wakayarejea yale yale waliyo katazwa. Na wakawa akija Mtume s.a.w. wakimwamkia kwa maamkio ya kumuapiza. Ndiyo ikashuka Aya hii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, huwaoni, (ewe Mtume), Mayahudi waliokatazwa wasizungumze kwa siri maneno yanayowatia shaka Waumini, kisha wanarudi kufanya yale waliyokatazwa, na wanazungumza kwa siri maneno ya dhambi, uadui na kuenda kinyume na amri ya Mtume? Na wanapokujia hawa Mayahudi kwa jambo lolote miongoni mwa mambo, wanakuamkia kwa maamkizi ambayo siyo yale Allah Mtukufu Aliyoyafanya ni maamkizi yako, na wanasema, «As-sām ‘alayka» yaani, Mauti yakushukie! Na wanasema wakiambiana wao kwa wao, «Si Atuangamize Allah Mtukufu kwa yale tunayomuambia Muhammad, iwapo ni Mtume kikweli?» Moto wa Jahanamu utawatosha: wataungia na watalihisi joto lake, na ubaya wa marejeo ni huo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net