Al-Mujaadila 58:7
المجادلةأَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَـٰثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَآ أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا۟ ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا۟ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ
Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. [7]
[7] Kwani hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na yaliomo katika ardhi, na wala hapana siri ya watu watatu ila Yeye Mwenyezi Mungu ndiye wane wao kwa kuyajua kwake wanayo fanyia siri, wala hawawi watano ila na Yeye ndiye wa sita wao. Wala duni kuliko hivyo, wala kuzidi hivyo, ila Yeye yuko pamoja nao, anayajua hayo wanayo yanong'ona, popote walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawapa khabari kwa kila walilo litenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ujuzi wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hujui kwamba Allah Mtukufu Yuwajua kila kitu kilicho mbinguni na ardhini? Hawanong’oni watu watatu, kati ya viumbe Vyake, maneno ya siri isipokuwa Allah Mtukufu ni wanne wao, wala watano isipokuwa Yeye ni wa sita wao, wala wachache kuliko idadi hiyo iliyotajwa wala wengi kuliko idadi hiyo isipokuwa Yeye Huwa Yuko pamoja nao kwa ujuzi wake, mahali popote walipo. Hakuna chochote kinachofichika Kwake kuhusu mambo yao. Kisha Allah Mtukufu Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, Atawapa habari ya kile walichokifanya chema au kibaya, na Atawalipa kwa walichokifanya. Hakika Allah Mtukufu kwa kila kitu ni Mjuzi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net