Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 6

Al-Mujaadila 58:6

المجادلة

يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓا۟ ۚ أَحْصَىٰهُ ٱللَّهُ وَنَسُوهُ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ

Maana

Siku atakapowafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyoyatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku atapo wafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyo yatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu. [6]

[6] Siku Mwenyezi Mungu atapo wafufua wote baada ya kwisha kufa kwao, na awape khabari za yale waliyo yatenda. Mwenyezi Mungu amewawekea yote na ameyahifadhi, na wao wameyasahau. Na Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa yote na anayajua yote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, (ewe Mtume), Siku ya Kiyama, Siku ambayo Allah Mtukufu Atawafufua wafu wote na Atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho katika uwanja mmoja, Awape habari ya yale waliyoyafanya ya kheri na shari. Allah Mtukufu Ameyadhibiti hayo na Ameyaandika katika Ubao Uliohifadhiwa, na Amewatunzia katika kurasa za matendo yao na hali wao wameyasahau. Na Allah Mtukufu ni Shahidi wa kila jambo, hakuna chochote kinachofichika Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net