Al-Mujaadila 58:5
المجادلةإِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ كُبِتُوا۟ كَمَا كُبِتَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَقَدْ أَنزَلْنَآ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ ۚ وَلِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ
Hakika wanaopinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao. Na tulikwishateremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao pinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale walio kuwa kabla yao. Na tulikwisha teremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha. [5]
[5] Hakika wanao mfanyia inda Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kupingana nao watatupiliwa mbali kama walivyo tupiliwa mbali walio kuwa kabla yao. Na Sisi tumekwisha teremsha dalili zilizo wazi za kuonyesha Haki. Na hao wapinzani watapata adhabu ya kuwafedhehesha mno.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale wanaomfanyia uadui Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakaenda kinyume na amri zake, watadhalilishwa na watatwezwa kama walivyodhalilishwa ummah waliokuwa kabla yao waliopingana na Allah Mtukufu na Mitume Wake. Na tumeteremsha aya zenye hoja zilizo wazi zinazoonyesha kuwa Sheria ya Allah Mtukufu na mipaka Yake ni kweli. Na wenye kuzikanusha aya hizo watapata adhabu yenye kudhalilisha ndani ya moto wa Jahanamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net