Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 10

Al-Mujaadila 58:10

المجادلة

إِنَّمَا ٱلنَّجْوَىٰ مِنَ ٱلشَّيْطَـٰنِ لِيَحْزُنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَلَيْسَ بِضَآرِّهِمْ شَيْـًٔا إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Maana

Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe wale walioamini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe walio amini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini. [10]

[10] Hakika kusema siri kwa kuchochea shaka shaka ni katika kuzainishwa na Shetani, ili apate kuingiza huzuni katika nyoyo za Waumini. Wala hayo hayawezi kuwaletea madhara yoyote wao ila kwa kupenda Mwenyezi Mungu. Basi Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu peke yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika kuzungumza kwa siri maneno ya dhambi na uadui ni katika ushawishi wa Shetani. Yeye ndiye anayeyapamba na kuyahimiza ili atie masikitiko kwenye nyoyo za Waumini. Na hilo halikuwa ni lenye kuwaudhi Waumini kitu chochote isipokuwa kwa matakwa ya Allah Mtukufu Aliyetukuka. Na kwa Allah Mtukufu na wajiegemeze wenye kumuamini katika mambo yao yote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net