Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 11

Al-Mujaadila 58:11

المجادلة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا۟ فِى ٱلْمَجَـٰلِسِ فَٱفْسَحُوا۟ يَفْسَحِ ٱللَّهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ ٱنشُزُوا۟ فَٱنشُزُوا۟ يَرْفَعِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ دَرَجَـٰتٍ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

Maana

Enyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: "Ondokeni", basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu, na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. [11]

[11] Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Mkitakiwa baadhi yenu kuwafanyia nafasi wenzenu mnapo kaa katika majlisi zenu, basi wafanyieni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkitakiwa kuondoka pale mlipo kaa basi ondokeni. Mwenyezi Mungu hutukuza vyeo vya Waumini, na wale walio pewa ilimu kwa daraja nyingi. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Mkitakiwa mpeane nafasi kwenye mabaraza (sehemu za kukaa) basi peaneni nafasi (yani mumpe nafasi aliyechelewa naye akae), na mkifanya hivyo Allah Mtukufu Atawakunjulia nafasi duniani na Akhera. Na mkitakiwa kwenu, enyi Waumini, muinuke katika mabaraza yenu kwa jambo lolote lenye kheri kwenu, basi inukeni. Allah Mtukufu Anavipandisha vyeo vya Waumini miongoni mwenu, na Anavipandisha vyeo vya wenye elimu daraja nyingi kwa kuwapatia malipo mema na daraja za kupata radhi. Na Allah Mtukufu Anayatambua matendo yenu, hakuna chochote kinachofichika Kwake katika hayo, na Yeye ni mwenye kuwalipa nyinyi kwayo. Katika aya hii pana kutukuza cheo cha wanavyuoni na utukufu wao na kutukuzwa daraja zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net