Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 2

Al-Mujaadila 58:2

المجادلة

ٱلَّذِينَ يُظَـٰهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَآئِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَـٰتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَـٰتُهُمْ إِلَّا ٱلَّـٰٓـِٔى وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ ٱلْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ

Maana

Wale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa. Na hakika hao wanasema neno ovu mno, na la uongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi mno, Mwenye kusamehe zaidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale miongoni mwenu wanao watenga wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa. Na hakika hao wanasema neno linalo chusha, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria, Mwenye kusamehe. [2]

[2] Enyi Waumini! Hao miongoni mwenu wanao jitenga na wake zao kwa kuwashabihisha katika kuharimikiana nao kuwa ati ni kama mama zao, ni wakosa. Wake zao sio mama zao. Ukitaka haki mama zao ni wale walio wazaa tu. Na hakika wanao watenga wake zao kwa kusema hivyo wanasema kauli inayo chusha, inayo udhi katika murwa mwema, na ni uwongo ulio tokana na haki. Na hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mkuu wa kusamehe na kughufiria kwa yaliyo kwisha pita kwenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale wanaowafananisha wake zao na mama zao, kwa kutoka mwanamume miongoni mwao kumwambia mkewe, «Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu» yaani kuwa kumuingilia ni haramu, wamemuasi Allah Mtukufu na wameenda kinyume na Sheria. Na wake zao si mama zao kihakika, bali wao ni wake zao; mama zao ni wale tu waliowazaa. Na hawa wanaowafananisha wake zao na mama zao, kwa hakika, wanasema neno la urongo lililo baya lisilo sahihi. Na hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamahe na kusitiri kwa wale ambao yametokea kwao baadhi ya mambo ya uvunjaji Sheria kisha wakayarakebisha kwa kutubia kidhati.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net