Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 3

Al-Mujaadila 58:3

المجادلة

وَٱلَّذِينَ يُظَـٰهِرُونَ مِن نِّسَآئِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا۟ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَآسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِۦ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

Maana

Na wale wanaojitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyoyasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda. [3]

[3] Na wale wanao watenga wake zao na kisha wakarejeza kauli yao, wakayaona makosa yao, na wakataka kubaki na wake zao, basi juu yao kumkomboa mtumwa kabla ya kugusana. Hayo aliyo yawajibisha Mwenyezi Mungu, ya kukomboa mtumwa, ni mawaidha kwenu mnawaidhiwa ili msirejee tena katika makosa hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua vilivyo myatendayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanaojiharamishia wake zao kwa kuwafananisha na migongo ya mama zao kisha wakarudi nyuma na hilo neno na wakataka kuwaingilia, basi ni juu ya yule mume aliyetoa tamshi la ẓihār, katika hali hii, atoe kafara ya kule kujiharamishia, nayo ni kuacha huru mtumwa muumini au kijakazi, kabla hajamuingilia yule mkewe aliyemfananisha na mgongo wa mama yake. Hiyo ndiyo hukumu ya Allah Mtukufu kwa anayemfananisha mkewe na mgongo wa mama yake, mnakumbushwa muwaidhike nayo, (enyi Waumini), ili msiingie kwenye kosa la kuwafananisha wake zenu na mama zenu na kusema neno la uzushi, na mtoe kafara mnapoingia kwenye kosa hilo, na ili msirudie tena kufanya hilo. Na Allah Mtukufu hakifichiki chochote Kwake katika matendo yenu, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net