Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 57 · Aya ya 4

Al-Hadid 57:4

الحديد

هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Maana

Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akainuka akawa juu ya Kitu cha Enzi. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akakaa vyema juu ya enzi. Anayajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni, na yanayo panda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayo yatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi, kisha Akawa juu ya ‛Arsh Yake, iliyo juu ya viumbe Vyake vyote, kuwa Juu kunakonasibiana na utukufu Wake. Anavijua vinavyoingia ardhini, miongoni mwa mbegu, mvua na visivyokuwa hivyo, na vinavyotoka humo miongoni mwa mimea, nafaka na matunda, na vinavyoshuka kutoka mbinguni, miongoni mwa mvua na vinginevyo, na vinavyopanda huko, miongoni mwa Malaika na matendo (ya waja), na Yeye, kutakasika ni Kwake, Yuko pamoja na nyinyi kwa ujuzi Wake popote mnapokuwa. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyaona matendo yenu mnayoyafanya na Atawalipa kwayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hadid

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net