Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 57 · Aya ya 3

Al-Hadid 57:3

الحديد

هُوَ ٱلْأَوَّلُ وَٱلْـَٔاخِرُ وَٱلظَّـٰهِرُ وَٱلْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhahiri na wa Siri, naye ndiye ajuaye zaidi kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye wa Mwanzo Ambaye hakukuwa na chochote kabla Yake, na Ndiye wa Mwisho Ambaye hakuna kitu chochote baada Yake, na Ndiye Aliyejitokeza Ambaye hakuna kitu chochote juu Yake, na Ndiye wa ndani Ambaye hakuna kitu chochote kilicho karibu kuliko Yeye, na hakuna chochote kinachofichika Kwake ardhini wala mbinguni, na Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hadid

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net