Al-Hadid
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ 4
{4} "Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita." Ya kwanza yake ni Jumapili na ya mwisho yake ni Ijumaa "kisha akainuka juu ya Kitu cha enzi" kuinuka kunakolingana na utukufu wake juu viumbe vyake vyote. "Anayajua yanayoingia katika ardhi" kama vile nafaka, wanyama, mvua na mengineyo. "Na yanayopanda kutoka humo" kama vile mimea, miti, wanyama na mengineyo "na yanayoteremka kutoka mbinguni" kama vile Malaika, mipango yake na riziki. "Na yanayopanda humo" kama vile Malaika, roho, na dua, matendo na vitu vinginevyo. "na Yeye yu pamoja nanyi popote mlipo." Kama vile kauli yake: "Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo." Na upamoja wake huu ni kwa elimu yake na kuona kwake. Ndiyo maana akatishia kwa adhabu na akaahidi ahadi ya kulipa kulingana na matendo, kwa kauli yake: "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno mnayoyatenda." Yaani, Yeye Mtukufu anayaona mno matendo mnayoyafanya na yaliyoyasababisha; ya wema na maovu, kisha atakulipeni kwa hayo na amekulindieni.