Al-Qamar 54:8
القمرمُّهْطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِ ۖ يَقُولُ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: 'Hii ni siku ngumu.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu. [8]
[8] Wakimkimbilia huyo mwitaji, wakimtazama kwa unyonge na unyenekevu, macho yao yanamwangalia yeye tu. Makafiri watasema Siku ya Kiyama: Hii leo ni siku nzito, siku ya shida!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hali ya kukimbilia kile walichoitiwa. Hapo waseme makafiri, «Hii ni siku nzito yenye vitisho vikubwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net