Al-Qamar 54:9
القمركَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا۟ عَبْدَنَا وَقَالُوا۟ مَجْنُونٌ وَٱزْدُجِرَ
Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. [9]
[9] Kabla ya makafiri wa Makka walikwisha kanusha kaumu ya Nuhu. Walimkadhibisha Nuhu, mja wetu na Mtume wetu, wakamsingizia kuwa ana wazimu. Wakaingiza baina yake na kufikisha kwake Ujumbe kila namna ya maudhi na vitisho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walikanusha kabla ya watu wako, (ewe Mtume), watu wa Nûḥ wakamkanusha mja wetu Nûḥ na wakasema, «Yeye ni Mwendawazimu.» Wakamkaripia huku wakimtisha kwa aina nyingi za mateso iwapo hatakomeka na ulinganizi wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net