Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 54 · Aya ya 7

Al-Qamar 54:7

القمر

خُشَّعًا أَبْصَـٰرُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُّنتَشِرٌ

Maana

Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige waliotawanyika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika! [7]

[7] Macho yao yatainamia chini kwa wingi wa kitisho, wakitoka makaburini kama kwamba ni nzige walio tawanyika, kwa wingi wao na mbio zao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hali yakuwa macho yao yamedhalilika, wanatoka makaburini kana kwamba kwa kuenea kwao na upesi wa kuenda kwenye kuhesabiwa, ni nzige walioenea angani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qamar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net