Al-Qamar 54:6
القمرفَتَوَلَّ عَنْهُمْ ۘ يَوْمَ يَدْعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَىْءٍ نُّكُرٍ
Basi jiepushe nao. Siku atakapoita mwitaji kuliendea jambo linalochusha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; . [6]
[6] Ewe Muhammad! Waachilie mbali hawa makafiri, nawe ngojea siku atapoita mwitaji wa Mwenyezi Mungu kuitia jambo ambalo nafsi inalichukia mno!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hivyo, wapuuze, (ewe Mtume), na uingojee Siku Malaika Atakapoita, kwa kupuliza kwenye baragumu, kwenye jambo linalotisha linalochukiza, nalo ni Kisimamo cha Hesabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net