Al-Qamar 54:2
القمروَإِن يَرَوْا۟ ءَايَةً يُعْرِضُوا۟ وَيَقُولُوا۟ سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ
Na wakiona Ishara, hugeuka upande na husema: 'Huu uchawi tu unazidi kuendelea.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea. [2]
[2] Na makafiri wakiona Ishara, yaani muujiza mkubwa, wao hupuuza wakaacha kuuamini. Bali husema: Huu ni uchawi wa daima unaendelea!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na washirikina wakiiona dalili na ushahidi wa ukweli wa Mtume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), wanakataa kuziamini na kuzisadiki hali ya kukanusha na kupinga, na wanasema baada ya dalili kujitokeza, «Huu ni uchawi wenye ubatilifu na wenye kuondoka na kupotea usiokuwa na sifa ya kudumu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net