Al-Qamar 54:1
القمرٱقْتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلْقَمَرُ
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! [1]
[1] Kiyama kimekaribia na mwezi utapasuka hapana hivi wala hivi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kimekaribia Kiyama na mwezi umepasuka pande mbili, (pale makafiri wa Makkah walipomtaka Nabii, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, awaoneshe alama), na yeye akamuomba Allah Mtukufu na akawaonesha hiyo alama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net