At-Tur 52:29
الطورفَذَكِّرْ فَمَآ أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ
Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. [29]
[29] Wewe endelea na kukumbusha kama unavyo fanya. Kwani wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu aliyo kuneemesha kukupa Unabii na akili iliyo timia, si kuhani anaye toa khabari za ghaibu bila ya ilimu, wala si mwendawazimu unaye sema usiyo yasadiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi wakumbushe (ewe Mtume), wale uliotumwa kwao kwa hii Qur’ani, kwani hukuwa wewe, kwa neema ya Allah Mtukufu Aliokuneemesha kwayo ya unabii na busara ya akili, ni kuhani anayetoa habari za ghaibu bila ujuzi, wala mwendawazimu asiyejua analolisema, kama wanavyodai.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net