Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 52 · Aya ya 28

At-Tur 52:28

الطور

إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْبَرُّ ٱلرَّحِيمُ

Maana

Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu. [28]

[28] Hakika sisi kabla ya haya tulikuwa duniani tukimuabudu Yeye tu. Yeye peke yake ndiye Mhisani Mkunjufu wa rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sisi tulikuwa, hapo kabla, tukimnyenyekea na kumuomba yeye Peke Yake, Atulinde na adhabu ya vuke la Motoni na Atupeleke kwenye starehe ya Peponi, Allah Mtukufu Akatukubalia maombi yetu, na Akatupa tulichokiomba. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kheri, Mwenye kurehemu. Na miongoni mwa wingi wa kheri Zake na rehema Zake kwetu ni kule kutupa radhi zake na Pepo, na kutuepusha na hasira Zake na Moto.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tur

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net