Adh-Dhaariyat 51:24
الذارياتهَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْمُكْرَمِينَ
Je, imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanaoheshimiwa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? [24]
[24] Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je imekujia (ewe Mtume), habari ya wageni wa Ibrãhîm aliyewakirimu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net