Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 51 · Aya ya 23

Adh-Dhaariyat 51:23

الذاريات

فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِنَّهُۥ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَآ أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ

Maana

Basi ninaapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. [23]

[23] Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Anaapa Allah Mtukufu kwa dhati Yake tukufu kwamba kile Alichowaahidi ni kweli, msikifanyie shaka kama ambavyo hamshuku kuwa nyinyi mnasema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Adh-Dhaariyat

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net