Adh-Dhaariyat 51:25
الذارياتإِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَـٰمًا ۖ قَالَ سَلَـٰمٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
Walipoingia kwake na wakasema: 'Salama!' Na yeye akasema: 'Salama! Nyinyi ni watu nisiowajua.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. [25]
[25] Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walikuwa ni miongoni mwa Malaika watukufu-wakati walipomjia nyumbani kwake wakamuamkia kwa kumuambia, «Salama!»Akawarudishia maamkizi kwa kusema, «Salama ni kwenu! Nyinyi ni watu wageni hatuwajui».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net