Adh-Dhaariyat 51:20
الذارياتوَفِى ٱلْأَرْضِ ءَايَـٰتٌ لِّلْمُوقِنِينَ
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. [20]
[20] Na katika ardhi zipo dalili nyingi zilizo wazi zinazo pelekea yakini, kwa mwenye kuitafuta njia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na katika ardhi kuna mazingatio na dalili za wazi za uwezo wa Allah Mtukufu kwa watu wenye yakini kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki, (Aliye Peke Yake na asiye na mshirika), na wenye kumuamini Mtume Wake. (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net