Adh-Dhaariyat 51:19
الذارياتوَفِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiyeomba.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. [19]
[19] Na katika mali yao wakiweka fungu maalumu lilio thibiti kwa ajili ya wenye haja, wanao omba na wanao jizuilia kuomba kwa kujiteta.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na katika mali zao kulikuwa na fungu la zaka wanalitoa, na pia fungu lisilo la zaka, huwapa wahitaji wanaowaomba na wasiowaomba kwa kuona haya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net