Adh-Dhaariyat 51:21
الذارياتوَفِىٓ أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Na pia katika nafsi zenu - Je, hamwoni?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? [21]
[21] Na hali kadhaalika katika nafsi zenu zipo Ishara zilizo wazi. Je! Mmeghafilika nazo, hamzioni?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na katika kuwaumba nyinyi kuna dalili za uwezo wa Allah Mtukufu Aliyetukuka, na kuna mazingatio ya kuwaonyesha nyinyi upweke wa Muumba wenu, na kwamba hakuna Mola Anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Je, mumeghafilika na hilo mkawa hamlioni mkazingatia kwalo?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net