Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 50 · Aya ya 45

Qaaf 50:45

ق

نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ۖ فَذَكِّرْ بِٱلْقُرْءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ

Maana

Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-ani anayeliogopa onyo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo. [45]

[45] Sisi tunajua kuliko yeyote hayo wayasemayo ya uwongo juu yaliyo khusu Utume wako. Wala wewe hukutumwa uwalazimishe kwa unayo yataka. Ila wewe ni mwonyaji basi mkumbushe kwa Qur'ani Muumini mwenye kuiogopa adhabu yangu ili ukumbusho umfae..

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sisi ni wajuzi zaidi kwa wanayoyasema hawa washirikina, ya kumzulia Allah Mtukufu urongo na kukanusha aya Zake. Na hukuwa wewe, (ewe Mtume), umepewa nguvu juu yao ya kuwalazimisha waingie katika Uislamu, hakika ni kwamba wewe umetumwa uwe mfikishaji. Basi mkumbushe kwa Qur’ani anayeogopa onyo langu, kwa kuwa asiyeogopa onyo (la Allah Mtukufu) hafaidiki kwa kukumbushwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Qaaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net