Adh-Dhaariyat 51:1
الذارياتوَٱلذَّٰرِيَـٰتِ ذَرْوًا
Ninaapa kwa pepo zinazotawanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naapa kwa pepo zinazo tawanya! [1]
[1] Ninaapa kwa pepo zinazo timua mawingu, zikayasukuma kwa nguvu, huku zikibeba mizigo mizito ya maji, zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu, zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anaapa kwa upepo wenye kurusha mchanga.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net