Qaaf 50:44
قيَوْمَ تَشَقَّقُ ٱلْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ۚ ذَٰلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ
Siku itapowapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi. [44]
[44] Siku itakapo wapasukilia ardhi, na watoke humo mbio mbio wakikimbilia mkutanoni...Hilo jambo kuu la kuwakusanya wote ni dogo na jepesi kwetu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Siku ambayo ardhi itapasukapasuka itoe wafu waliozikwa humo, watoke mbio kuelekea upande wa yule anayeita. Kuwakusanya watu hivyo kwenye Kisimamo cha Hesabu ni jambo sahali kwetu na rahisi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net