Qaaf 50:25
قمَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ
Akatazaye mno heri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka, [25]
[25] Na akapita mipaka kuzuia kheri, mwenye kudhulumu akaipindukia Haki, mwenye kumtilia shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu na aliyo yateremsha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwenye kuzuia kutekeleza haki zilizo juu yake katika mali yake, anaye wadhulumu waja wa Allah Mtukufu na kukiuka mipaka Yake, anayelifanyia shaka agizo la Allah Mtukufu na onyo Lake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net