Qaaf 50:24
قأَلْقِيَا فِى جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ
Mtupeni katika Jahanamu kila kafiri mkubwa mkaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda, [24]
[24] Malaika wawili wataambiwa: Watieni katika Jahannamu kila aliye pita mipaka kwa ukafiri, na aliye pita mipaka kwa inadi, na akaacha kuifuata Haki,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Aseme kuwaambia Malaika wawili: mwenye kuongoza na yule shahidi, baada ya kutolewa uamuzi baina ya viumbe, «Mtupeni ndani ya Jahanamu kila mwenye kukataa kuwa Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki, aliye mwingi wa ukafiri na ukanushaji, mwenye kuipinga haki».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net