Qaaf 50:23
قوَقَالَ قَرِينُهُۥ هَـٰذَا مَا لَدَىَّ عَتِيدٌ
Na mwenzake atasema: 'Huyu niliye naye mimi keshatayarishwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa. [23]
[23] Na Shetani wake aliye kuwa mwongozi wake duniani, atasema: Kafiri huyu alioko kwangu yuko tayari kuingia Jahannamu kwa kupotezwa nami.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Malaika muandishi mwenye kumtolea ushahidi atasema, «Haya ndiyo niliyonayo kutoka kwenye rikodi ya matendo yake. Nayo imetayarishwa, imehifadhiwa na ipo hapa kwangu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net