Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 50 · Aya ya 22

Qaaf 50:22

ق

لَّقَدْ كُنتَ فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلْيَوْمَ حَدِيدٌ

Maana

(Aambiwe): 'Kwa hakika ulikuwa umeghafilika mbali na haya. Basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali mno.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali. [22]

[22] Wataambiwa, kumtisha huyo mwenye kukadhibisha: Hakika wewe huko duniani ulikuwa umeghafilika kabisa na haya unayo sononeka nayo hivi sasa. Basi Sisi tumekuondolea pazia lilio kuwa likikuzuia usiyaone mambo ya Akhera. Basi jicho lako hii leo linaona kwa nguvu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika ulikuwa katika kughafilika na tukio hili unaloliona leo, (ewe binadamu), ndipo tukakifunua kifuniko chako kilichoziba moyo wako, kughafilika kukakuondokea, basi leo macho yako, katika kile unachokitolea ushahidi, ni makali.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Qaaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net