Qaaf 50:26
قٱلَّذِى جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِى ٱلْعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ
Aliyeweka mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali. [26]
[26] Aliye mfanya mungu mwengine wa kumuabudu pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni huyo katika adhabu yenye mwisho wa ukali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Aliyemshirikisha Allah Mtukufu kwa kukiabudu kiabudiwa kingine miongoni mwa viumbe Vyake pamoja na Yeye. Mtupeni ndani ya adhabu ya moto wa Jahanamu ulio mkali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net