Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 99

Al-Maaida 5:99

المائدة

مَّا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ

Maana

Hakuna kilicho juu ya Mtume isipokuwa kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnachokidhihirisha na mnachokificha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haimlazimu Mtume ila kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnacho kidhihirisha na mnacho kificha. [99]

[99] Haimlazimikii Mtume ila kuwafikishia watu anayo funuliwa yeye, ili isimame hoja juu yao na wasiwe na kisingizio chochote cha kuwa ati hawakuonywa wala hawakufunzwa. Basi yajueni anayo kuleteeni Mtume, kwani Mwenyezi Mungu anayajua mnayo dhihirisha na mnayo yaficha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anawaelezea kwamba shughuli ya Mtume Wake, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni kuongoza kwa kuelekeza na kufikisha na kwamba uongofu wa taufiki uko mkononi mwa Allah Mtukufu, Peke Yake, na kwamba mambo yaliyomo ndani ya nafsi za watu, katika yale wanayoyafanya kwa siri na wanayoyatangaza, ya uongofu na upotevu, Allah Mtukufu Anayajua.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net