Al-Maaida 5:98
المائدةٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ وَأَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu. [98]
[98] Enyi watu! Jueni kuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali, humteremkia anaye halalisha vya haramu, naye pia ni Mwingi wa kusamehe dhambi za mwenye kutubu na akaingia kumt'ii. Naye ni Mwenye rehema sana, na kwa hivyo hamchukulii mtu papo kwa papo kwa kila alitendalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Jueni, enyi watu, kwamba Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, ni Mkali wa mateso kwa anayemuasi na kwamba Allah Mtukufu ni Mwingi wa Kusamehe, ni Mwingi wa rehema kwa anayetubia na kurejea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net