Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 100

Al-Maaida 5:100

المائدة

قُل لَّا يَسْتَوِى ٱلْخَبِيثُ وَٱلطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ ٱلْخَبِيثِ ۚ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Maana

Sema: Haviwi sawa viovu na vizuri hata kama utapendezwa na wingi wa viovu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili ya hali ya juu, ili mfaulu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Haviwi sawa viovu na vyema ujapo kupendeza wingi wa viovu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, ili mpate kufanikiwa. [100]

[100] Ewe Nabii! Waambie watu: Si sawa sawa vile vizuri anavyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu na vibaya anavyo kuharimishieni. Kwani farka iliyo baina ya viwili hivyo kwa Mwenyezi Mungu ni kubwa, na hata hivyo vibaya vingawa ni vingi na vinawapendeza watu wengi. Basi enyi wenye akili! Ufanyeni ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu uwe ni kinga yenu isikupateni adhabu yake kwa kukhiari vilivyo vyema, na kujiepusha na viovu, ili mpate kuwa miongoni walio fuzu duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, «Hakilingani kiovu na chema cha kila kitu»: Kafiri halingani na Muumini, mwenye kuasi halingani na mtiifu, mjinga halingani na mjuzi, na mwenye kufanya uzushi halingani na mwenye kufuata njia sahihi na mali ya haramu hayalingani na ya halali, ingawa unakuvutia wewe, ewe binadamu, wingi wa viovu na idadi kubwa ya watu wake. Basi mcheni Allah Mtukufu, enyi wenye akili bora, kwa kujiepusha na machafu na kufanya mazuri, mpate kufuzu kwa kulifikia lengo kubwa, nalo ni radhi ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na kufaulu kupata Pepo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net