Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 101

Al-Maaida 5:101

المائدة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَسْـَٔلُوا۟ عَنْ أَشْيَآءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْـَٔلُوا۟ عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلْقُرْءَانُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا ٱللَّهُ عَنْهَا ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ

Maana

Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo mkidhihirishiwa, yatawachukiza. Na mkiuliza juu yake wakati inateremshwa Qur-ani, mtadhihirishiwa hayo. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mpole.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole. [101]

[101] Enyi mlio amini! Msimuulize Nabii mambo ambayo Mwenyezi Mungu amekuficheni mkataka yafichuliwe, na mkamuuliza Nabii katika uhai wake, kwani Qur'ani inamteremkia bado. Na Mwenyezi Mungu atakubainishieni itapo hitajika. Mwenyezi Mungu amekusameheni kwa yasiyo tajwa, hatokuadhibuni kwayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye wasaa katika upole. Basi hana papara katika kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu, Mtume wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiulize mambo ya Dini ambayo hamkuamrishwa chochote kuhusu hayo, kama kuuliza kuhusu mambo ambayo hayajatokea au yale ambayo yatapelekea mikazo ya Sheria ambayo lau mngekalifishwa nayo yangalikuwa ni magumu kwenu, na lau mngeyauliza wakati wa uhai wa Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,, wakati Qur’ani inateremka, mungalielezewa, na pengine mkakalifishwa nayo na mkalemewa nayo. Hayo Allah Mtukufu Ameyaacha ili kuwapumzisha waja Wake nayo. Na Allah Mtukufu ni Msamehefu sana kwa waja wake wanapotubia, ni Mpole sana kwao, Hawaadhibu wakirudi Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net