Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 102

Al-Maaida 5:102

المائدة

قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا۟ بِهَا كَـٰفِرِينَ

Maana

Hakika, walikwishayauliza kaumu ya kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakufuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Waliyauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakataa. [102]

[102] Katika jamaa walio kutangulieni walikuwapo walio uliza mfano wa haya, mambo mazito mazito; na Manabii wao walipo wakalifisha ya kufanya wakaona mazito kuyatenda, wakayaacha, na wakawa ni wenye kuyakanya. Kwani Mwenyezi Mungu hupendelea wepesi, wala hapendelei uzito; na huwakalifisha watu kwa wanayo yaweza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mfano wa maswali hayo, waliwahi waliokuwa kabla yenu kuwauliza Mitume wao. Walipoamrishwa yale waliokuwa wakiyauliza waliyakanusha na wasiyatekeleze. Basi, tahadharini msiwe kama wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net