Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 96

Al-Maaida 5:96

المائدة

أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ ٱلْبَحْرِ وَطَعَامُهُۥ مَتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ ٱلْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِىٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Maana

Mmehalalishiwa mawindo ya baharini na kuyala, kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya barani maadamu mko katika Ihram. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini na kuvila, kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya wanyama wa bara maadamu mmeharimia Hija. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake. [96]

[96] Mwenyezi Mungu amekuhalalishieni kuvua wanyama wa baharini, na muwale, na wanufaike kwao wakaazi wenyeji na wasafiri. Na amekuharimishieni kuwinda wanyama wa bara wasio fugwa kwa kawaida majumbani, katika muda ule unapo kuwa katika Hija au Umra, kwenye eneo takatifu linalo itwa Alharam. Na mzingatieni Mwenyezi Mungu, na iogopeni adhabu yake. Basi msende kinyume naye, kwani nyinyi mtarejea kwake Siku ya Kiyama, na hapo atakulipeni kwa yote mliyo yatenda. (Huu ni mfano katika mifano mingi ya Uislamu tangu hapo kale unavyo pendelea kulinda tabia ya mazingara kwa kuhifadhi wanyama wasiuliwe ovyo, na miti isikatwe ovyo, na hata maji ya mito na maziwa yasitumiwe kwa fujo, kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wafujaji!)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Amewahalalishia, enyi Waislamu, mtapokuwa kwenye hali ya ihramu, viwindwa wa baharini, nao ni wale wavuliwao baharini wakiwa hai, na chakula chake, nacho ni kiumbe kilichokufa kitokacho humo, kwa ajili mnufaike mkiwa ni wakazi au ni wasafiri. Na Ameharamishia viwindwa wa barani mkiwa mko kwenye ihramu ya Hija au ya Umra. Na muogopeni Allah Mtukufu na mtekeleze amri Zake zote na mjiepushe na makatazo Yake yote, mpaka mfuzu kwa thawabu Zake kubwa na msalimike na ukali wa mateso Yake mnapofufuliwa ili mhesabiwe na mlipwe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net