Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 95

Al-Maaida 5:95

المائدة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَقْتُلُوا۟ ٱلصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُۥ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَآءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ ٱلنَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِۦ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًۢا بَـٰلِغَ ٱلْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّـٰرَةٌ طَعَامُ مَسَـٰكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِۦ ۗ عَفَا ٱللَّهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ ٱللَّهُ مِنْهُ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ ذُو ٱنتِقَامٍ

Maana

Enyi mlioamini! Msiwaue mawindo hali ya kuwa mko katika Ihram (ya Hija au 'Umra). Na miongoni mwenu atakayemuua makusudi, basi malipo yake yatakuwa ni kuchinja kilicho sawa na alichokiua, katika mifugo, kama wanavyohukumu hivyo waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al-Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwishayafuta yaliyopita. Lakini atakayefanya tena, Mwenyezi Mungu atamwadhibu vikali. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kuadhibu vikali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiue wanyama wa kuwinda nanyi mmeharimia katika Hija. Na miongoni mwenu atakaye muuwa makusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa kuchinja kilicho sawa na alicho kiuwa, katika mifugo, kama wanavyo hukumu waadilifu wawili miongoni mwenu. Mnyama huyo apelekwe kwenye Al Kaaba, au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili. Mwenyezi Mungu amekwisha yafuta yaliyo pita; lakini atakaye fanya tena Mwenyezi Mungu atampa adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu na Mwenye kuadhibu. [95]

[95] Enyi ambao mmeamini! Msiuwe nyama wa kuwinda nanyi mmenuia Hija na Umra na mmo kuzitimiliza. Na mwenye kumuuwa mnyama kama huyo kwa kukusudia basi itampasa atoe fidiya mfano wa mnyama aliye muuwa, ikiwa katika ngamia, ng'ombe au kondoo. Na hujuulikana huyo mfano wake kwa kukadiriwa na watu wawili waadilifu kati yenu, wahukumu na wawape mafakiri kwenye Al Kaaba, au atoe badala yake awape, au atoe chakula kadiri ya yule mnyama kuwapa mafakiri. Kila fakiri apewe chakula cha kumtosha kutwa yake. Hayo ndio kuondoa dhambi za kuwinda kuliko katazwa. Au badala ya hayo yote, afunge idadi ya siku za kadri ya wale masikini iliyo mbidi kuwalisha lau angewalisha. Na Mwenyezi Mungu amelazimisha hayo ili huyo mwenye kufanya lile kosa apate kuhisi matokeo ya kosa lake na uwovu wa malipo yake. Mwenyezi Mungu, lakini, amesamehe ukhalifu ulio tendekea kabla ya jambo hilo halijaharimishwa. Na mwenye kurejea tena kufanya uovu baada ya kujua kuwa ni haramu, basi hakika Mwenyezi Mungu atampa adabu kwa kitendo chake, naye Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda hashindiki, Mkali wa kumuadhibu anaye kakamia kutenda dhambi. (Tunaona kuwa Uislamu ulianzisha kulinda mazingara, na utajiri wa asili tangu hapo kale. Kutokana na kuhifadhiwa wanyama na ndege wa porini huko Makka, ndio hii leo tunaona zipo nyanda na mapori yanayo hifadhiwa wanyama wake, kwa mujibu wa utaalamu wa kisasa.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mlimuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, msiue viwindwa wa barani na nyinyi muko kwenye ihramu ya Hija au Umra au mkawa muko ndani ya Haram. Na yoyote mwenye kuua kiwindwa yoyote kati ya viwindwa wa barani kwa kusudi, basi malipo yake ni achinje, miongoni mwa wanyama- howa: ngamia au ng’ombe au mbuzi na kondoo, anayefanana na kiwindwa huyo, baada ya waadilifu wawili kumfanyia makadirio, na amgawe kwa masikini wa eneo la Haram au anunue chakula kwa thamani ya mfano wake na awagawie masikini wa eneo la Haram, kila masikini nusu pishi au afunge, badala yake, siku moja kwa kila nusu pishi ya chakula hicho. Allah Mtukufu Ameyapasisha malipo haya, ili mkosa apate matokeo ya kitendo chake. Na wale ambao ilitokea kwao kufanya lolote kama hilo kabla ya kuharamishwa, basi Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ashawasamehe. Na yoyote mwenye kurudia uhalifu huo kwa kusudi, baada ya kuharamishwa, huyo amejihatarisha kupata mateso ya Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu ni Mwenye nguvu katika mamlaka Yake, na miongoni mwa nguvu zake ni kuwa Yeye atamtesa anayemuasi Akitaka, hakuna chenye kumzuia kufanya hivyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net